Virusi sawa na HIV ya paka vyagunduliwa Kenya
- 2 Juni 2016
Je unamiliki paka?
Taarifa hii bila shaka itakuwa yenye manufaa kwako.
Nchini Kenya, virusi hatari aina ya FIV, vinaavyofananana kabisa na virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi vimegunduliwa katika paka mmoja kupitia uchunguzi wa kimaabara.
Hii ni baada ya uchunguzi wa kina wa damu ya paka huyo kuthibitisha uwepo wa viini vinavyofanana kabisa na vile vinavyoathiri binaadamu.
Wafugaji wa paka na wanyama wa nyumbani wameonywa kuwapeleka wanyama wao kufanyiwa uchunguzi wa afya wanapowashuku wanyama wao wanaugua.
Virusi hivyo vinaitwa FIV (Feline Immunodefficiency Virus).
Ugonjwa huo sio mgeni katika wanyama.
Mwaka wa 1986 madaktari nchini Marekani waligundua virusi vilivyofanana kwa karibu na vile vinavyoambukiza binadamu vya HIV.
Lakini hii ndio mara ya kwanza kwa virusi hivyo kugunduliwa nchini Kenya.
Madaktari wa maabara ya Lancet mjini Nairobi Waligundua kuwa virusi hivyo vinasababisha ukosefu wa kinga mwilini na kudhoofisha afya ya wanyama hao wanaopendwa na kuishi majumbani.
Hata hivyo waliwahakikishia wafugaji wa paka kuwa hakuna ushuhuda wowowte wa maambukizi kutoka kwa paka hao kwenda kwa binadamu.
Daktari Dhaval Shah badala yake amewashauri wafugaji wa paka kuwafungia paka wao ndani ilikuwazuia wasijamiane na wale paka wanaorandaranda mitaani ambao huenda wameambukizwa ukimwi wa paka.
''kimsingi ugonjwa huu ni Ukimwi wa waka, japo inaambukizwa kupitia kwa mate na mkwaruzano haswa paka wanapopigana''
By Alchard_Kr
RC DAR ES SALAAM NA KOREA KUSINI WAWEKA JIWE LA MSINGI LA HOSPITALI YA CHANIKA MANISPAA YA ILALA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na Makamu wa Rais wa Shirika la Koica la nchini Korea Kusini, Taemyon Kwon, wakiweka tofali kwa pamoja kuashiria uweka wa jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika iliyopo Manispaa ya Ilala, inayojengwa kwa ufadhili wa nchi hiyo Dar es Salaam jana. Ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu sh. bilioni 8.8 za kitanzania.
Hutuba na taarifa ya mradi huo zilisomwa.
Balozi wa Korea nchini Geum-young Song (katikati), akizungumza katika hafla hiyo.
Wananchi wa Chanika wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali yao.
Diwani wa Kata ya Chanika, Mr Massaburi akitoa neno la Shukurani kwa RC Makonda, Serikali pamoja na Serikali ya Korea kwa ujenzi wa Hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mr Isaya (kulia), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victriana Ludovic na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo Mr Kim wakiweka jiwe la msingi la Hospitali hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanika wakiwa kwenye hafla hiyo.
Meneja wa Mradi huo, Mr Kim akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na ujembe wake ramani ya majengo ya Hospitali hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanika wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Wasanii wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Manispaa ya Ilala na Korea Kusini.SOMA ZAIDI>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Thank's