MICHEZO





TOTTENHAM WANAKIMBIZA MWIZI KIMYA KIMYA

Mabao ya Harry Kane na Dele Ali yalitosha kuiwezesha Tottenham kuongeza kasi na kuwakaribia kwa ukaribu Leicester ambao wali droo dhid ya West Ham, kwa ushindi huo Spurs wanafikisha alama 68 wakiwa wamecheza michezo 34 hiyo ambao zimebaki point kuwafikia Leicester.
 

Mshambuliaji mahiri wa kikosi cha Spurs Harry Kane alianza kuzifumania nyavu katika dakika ya tisa ya mchezo, kisha kiungo Delle Ali akaongeza bao la pili katika dakika ya 67 kipindi cha pili.,Katika dakika ya 71 Harry kane tena akawatungua Stoke City kabla ya Dele Ali kuhitimisha ushindi huo kwa bao la nne katika dakika ya 82.
 

Tottenham wakicheza ugenini katika dimba la Brittania wameibuka na ushindi huo wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City.



KOCHA MKUU WA TAIFA STARS KUREJEA YANGA

Imechapishwa na Gazeti la Habari Leo

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwassa
Mkwasa kurudi Yanga

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Mkwasa ameitwa kuongeza nguvu katika benchi la ufundi la Yanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri wiki ijayo.
Habari zilizopatikana jana kutoka Yanga, zilieleza kuwa tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshatoa ruhusa ili aweze kuisaidia Yanga kipindi hiki cha kuelekea mchezo huo. “Ni kweli Mkwasa ameitwa kuongeza nguvu, unajua Kocha wa Yanga (Hans Pluijm), anamkubali sana Mkwasa, hivyo wameona aje asaidie wakati huu ambapo hana majukumu Taifa Stars,” kilisema chanzo chetu na kusisitiza kwamba Mkwasa haina maana amejiondoa Taifa Stars.
Mkwasa hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, wala Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro na hata Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto. Hata hivyo, TFF iliwahi kutoa taarifa kwamba timu za Yanga na Azam zipo huru kuwatumia makocha wa Taifa Stars, Mkwasa na Hemed Morocco katika maandalizi yao kwa ajili ya michezo ya kimataifa inayowakabili.
Mkwassa alikuwa Kocha Msaidizi wa Yanga kabla ya kuteuliwa kuwa kocha muda wa Taifa Stars katikati ya mwaka uliopita akirithi mikoba ya Mholanzi Mart Nooij aliyetimuliwa baada ya matokeo mabaya ya Stars.
TFF ilisaini naye mkataba wa miezi 18 Oktoba mwaka jana baada ya kuridhishwa na kazi yake, ambapo mkataba huo utamalizika Machi 31 mwakani. Wakati huohuo, Mohammed Akida anaripoti kuwa Pluijm amesema ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda FC juzi utachangia kukiimarisha kikosi chake kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly mwishoni mwa wiki ijayo.
Yanga juzi ilishinda mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho, lakini haikuonesha kiwango cha kuvutia kiasi cha mashabiki kuingiwa na hofu kuhusu mchezo wao na Ahly.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Pluijm alikiri timu yake kucheza vibaya, lakini alisema hiyo ni moja ya mikakati yao kuhakikisha wanatunza nguvu za kucheza mechi zingine tatu zinazowakabili ikiwemo ya Al Ahly.
Pluijm alisema huo ni ushindi mkubwa kwao na sasa wanajipanga kushinda michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kabla ya kuikabili Al Ahly Jumamosi ijayo.
Kwa upande wake kocha wa Ndanda FC, Abdul Mingange, alisema kilichosababisha timu yake kupoteza mchezo huo ni kukosa uzoefu kwa wachezaji wake, ambao walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia. Mingange alisema timu yake ilicheza vizuri na kuutawala mchezo, lakini tatizo kubwa ilikuwa ni umaliziaji ambao ulikuwa kikwazo.
Bingwa wa michuano hiyo inayojulikana pia kama Kombe la FA, atawakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) mwaka 2017. Kutokana na ushindi huo, Yanga na Azam sasa zinaungana na Mwadui ya Shinyanga, ambayo Jumamosi iliifunga Geita Gold Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza mabao 3-0 na kufuzu nusu fainali. 
soma zaidi hapa katika gazeti la habari Leo ,habari nyingine zaid@>>>>>>>>


YANGA NA AZAM KUTINGA FA

YANGA NA AZAM KUTINGA FA
YANGA na Azam jana zilitinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kushinda michezo yao ya Robo Fainali.
Yanga ilikuwa mwenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo iliibuka Kidedea kwa mabao 2-1, wakati Azam ilikuwa mwenyeji wa Prisons Uwanja wa Azam Chamazi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Kutokana na ushindi huo, Yanga na Azam sasa zinaungana na Mwadui ya
Shinyanga, ambayo Jumamosi iliifunga Geita Gold Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza mabao 3-0 na kufuzu Nusu Fainali. Bingwa wa michuano hiyo inayojulikana pia kama Kombe la FA, atawakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
Katika mchezo wa jana, Ndanda ilikuwa ya kwanza kufanya shambulio la kushtukiza dakika ya sita wakati Atupele Green alipoukwamisha mpira wavuni, lakini mwamuzi alisema mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga, hali ambayo ililalamikiwa na wachezaji wa Ndanda.
Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu, huku Yanga ikipoteza nafasi nyingi zaidi kwa washambuliaji wake kushindwa kulenga lango. Yanga ilipata bao la kuongoza dakika ya 27 mfungaji akiwa Paul Nonga akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu wa Juma Abdul.
Ndanda FC ilisawazisha bao hilo dakika ya 56 mfungaji akiwa Kigi Makasy baada ya kuingia katika eneo la hatari na kupiga mpira uliomshinda kipa Deogratias Munishi ‘Dida’.
Yanga ilipata bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 69 mfungaji akiwa Kelvin Yondani, baada ya beki Paul Ngalema kumchezea madhambi Simon Msuva aliyekuwa akienda langoni, ambapo kutokana na faulo hiyo Ngalema alioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Jimmy Fanuel wa Shinyanga.
Katika mchezo wa Azam, washindi walianza kupata bao la kwanza dakika ya tisa mfungaji akiwa Shomary Kapombe aliyemalizia kazi nzuri ya Didier Kavumbagu.
Kapombe aliifungia Azam bao la pili dakika ya 50, wakati Khamis Mcha aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi John Bocco ‘Adebayor’ alifunga bao la tatu dakika ya 86.


Robo Fainali nyingine ya michuano hiyo itakuwa Aprili 9 mwaka huu, wakati Simba itakapokuwa mwenyeji wa Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Thank's